Unaweza kuchagua idadi ya wageni wanaoweza kuweka nafasi kwenye nyumba yako kabla ya ada ya mgeni wa ziada kutozwa. Kwa hivyo, ikiwa idadi ya wageni ulioweka kwenye Tangazo lako ni 6, unaweza kutoza ada ya ziada kwa kila mgeni baada ya mgeni wa pili au wa tatu na kadhalika.
Ada yako mpya itatumika kwa nafasi zitakazowekwa katika siku zijazo pekee.
Ikiwa ungependa kuongeza ada ya mgeni wa ziada kwenye nafasi iliyowekwa ambayo imethibitishwa, utahitaji kumtumia mgeni wako mabadiliko ya safari ili kurekebisha bei.